top of page

Hadithi za mafanikio

Safari ya Isaya Silungwe kama mshiriki katika Mradi wa Boresha Maisha ya Vijana na Mkurugenzi wa Agri Youth Forum ni ya kuvutia. Hadithi ya Isaya ni ushuhuda wa nguvu ya mabadiliko inayoweza kupatikana kupitia programu maalum za vijana na athari chanya wanazoweza kuwa nazo kwa watu na jamii zao.

Isaya alishiriki kikamilifu katika mafunzo mbalimbali yaliyoandaliwa kupitia mradi wa Boresha Maisha ya Vijana, yakijumuisha mada muhimu kama usawa wa kijinsia, mawasiliano, mabadiliko ya hali ya hewa, minyororo ya thamani, na mfumo wa chakula endelevu. Mafunzo haya yalimwezesha kupata maarifa na ujuzi unaohitajika ili kua na mchango chanya katika sekta ya kilimo.

Moja ya  fursa ya kipekee iliyoipata Isaya ilikuwa nafasi ya kushiriki katika Wiki ya Vijana ya Kitaifa, iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Vijana kwa kushirikiana na Asasi za vijana ikiwemo Tanzania Youth Coalition (TYC) kupitia Mradi wa BoreshaMaishaYaVijana. Wakati wa tukio hili, Isaya alitumia fursa hiyo kuonyesha shughuli za shirika lake kupitia kizimba cha TYC.  Moja ya eneo la kimradi ambalo Agri Youth Forum wanalifanyia kazi ni kilimo, haswa kilimo cha zabibu na uzalishaji wa mvinyo, ambalo lilivuta macho ya washiriki wengi

 

Moja ya matokeo muhimu ya ushiriki wa Isaya ilikuwa kufunga makubaliano na duka kubwa mkoni babati, Kwa kusambaza masanduku 10 ya zabibu kila wiki, Isaya aliongeza soko la shirika lake na pia kuleta bidhaa za kilimo zilizozalishwa kwa kuzingatia ubora kwa watumiaji

Ushawishi na kujituma kwa Isaya hakukuishia kwenye shughuli za kilimo na biashara kwenye kizimba. Alipata nafasi ya kuchaguliwa kama mmoja wa wazungumaji wakuu katika mdahalo wakati wa Wiki ya Vijana ya Kitaifa 2023. Jukwaa hili lilmruhusu kushirikisha uzoefu wake, ufahamu, na hadithi ya mafanikio ya shirika lake. Uzalendo wa Isaya kwa kilimo na kujitolea kwake viligonga nyoyo za wasikilizaji

WhatsApp Image 2023-12-13 at 11.27.53 AM.jpeg

Kuongezea mafanikio yake, Isaya alipendekezwa kama mmoja wa muwaniaji  wa Tuzo zinazotolewa na  moja ya shirika la Vijana katika kategoria ya kilimo. Michango yake ya kipekee kwenye tasnia ilitambuliwa, na alitangazwa kuwa mshindi. Tuzo hii iliyostahiki ilisherehekea si tu mafanikio ya binafsi ya Isaya bali pia ilionyesha mwangaza kwa athari chanya ya mipango ya Agri Youth Forum katika kukuza tasnia ya kilimo yenye ubunifu na endelevu miongoni mwa vijana

WhatsApp Image 2023-12-13 at 10.02.35 AM (1).jpeg

Hadithi ya mafanikio ya Isaya inafaa kutumiwa na viongozi wachanga kwenye sekta ya kilimo kama chanzo cha hamasa. Kupitia ushiriki wake katika Mradi wa Boresha Maisha ya Vijana na fursa zilizotolewa na TYC, Isaya anabadilisha siyo tu maisha yake mwenyewe bali pia anachangia katika maendeleo ya jamii yake na sekta ya kilimo kwa ujumla.

WhatsApp Image 2023-12-13 at 10.02_edited.jpg
bottom of page